Wednesday, November 14, 2012

Timu ukishafulia



Timu ukishafulia, nani wa kusaidia,

Kelele hazitozaa, goli hilo kujakuwa,

Ushindi kuja kutwaa, kazi ngumu huja kuwa,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!



Wengi wanaotambua, timu ndio huanzia,

Kila mchezaji kuwa, nafasi anayofaa,

Hawa wakishaingia, uwanja huwaamkia,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!



Wanafunzi mkitia, uwanjani wakajaa,

Shule kujigeuizia, si mechi ya kutegemewa,

Udogo hoja haijawa, wakubwa wakazidiwa,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!



Mashabiki ni murua, timu kuishangilia,

Ila wachezaji njia, mahala pakupitia,

Utulivu wakitwaa, magoli yataingia,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!



Adili wakiijaa, kufunga hufanikiwa,

Haki wakiangalia, mechi huwapendelea,

Ukweli wakiujua, uongo mabli hukaa,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!



Rushwa wakishakimbia, kufungwa haitkuwa,

Wakishajaa tamaa, hujifunga wao pia,

Ikawa kubwa balaa, mkabaki kuzomewa,

Washangiliaji bure, timu ukishafulia!







No comments: