Wednesday, November 14, 2012

Binadamu akishindwa

Nafasi yake masaa, binadamu hajajua,

Na analoliamua, lilikwishaandikiwa,

Yeye tu anatumiwa, kuwa njia kupitia,

Binadamu akishindwa, hivi Ally atashindwa ?

Mola akilikataa, jambo haliwezi kuwa,

Hata ubabe kutumia, nguvu huja kuishiwa,

Likawa linalokuwa, silo unalotarajia,

Binadamu akishindwa, hivi Ally atashindwa ?

Yote tumeandikiwa, na vingine haijawa,

Usijie kujua, eti wewe watufaa,

Mpanda hujushushua, mshuka akaenziwa,

Binadamu akishindwa, hivi Ally atashindwa ?

Utukufu kujitia, uchafu hukuingia,

Tena ukakusambaa, kila mtu kuujua,

Ila dhaifu ukiwa, hutoacha barikiwa,

Binadamu akishindwa, hivi Ally atashindwa ?

No comments: