Wednesday, November 14, 2012

Tatu ya hatitriki


Swali nimelisikia, shabiki waulizia,

Magoli ya kuingia, hayo vipi yatakuwa,

Matatu yalobakia, nani atajifungia,

Tatu ya hatitriki, msafi au fisadi ?



Ni kando wanaokaa, majeshi wakatumia,

Mipira wakaachia, miguuni kupitia,

Na jasho wasiotoa, ila majibu kungojea?

Tatu ya hatitriki, msafi au fisadi ?



Ni pumzi wa kutoa, au fedha kugawia,

Hongo wakaichukua, magoli kuyaachia,

Tena bila ya kujua, zaidi wangepatiwa ?

Tatu ya hatitriki, msafi au fisadi ?



Au wema walokuwa, sasa tusiowajua,

Mazuri wanayolilia, nchi kuja ambulia,

Na nguvu wasotumia, na hila zenye balaa,

Tatu ya hatitriki, msafi au fisadi ?

No comments: