Wednesday, November 14, 2012

Asiyekuwa na nuru



Haya hawezi elewa, na nuru asiyekuwa,

Ardhi imeshushiwa, wachache sana kufaa,

Adili wanaojua, na tajwidi kutia,

Asiyekuwa na nuru, haya hawezi elewa !



Nia wanaoitia, kazini hawajaingia,

Mola akatangulia, nao nyuma kufatia,

Taa wataichukua, hadi kaburini kwingia,

Asiyekuwa na nuru, haya hawezi elewa !



Kila wanaloamua, misingi wakifatia,

Yumkini kujaliwa, huwa lishakubaliwa,

Vingine haitakuwa, katika hii dunia,

Asiyekuwa na nuru, haya hawezi elewa !

No comments: