Tuesday, November 8, 2011

Dini ya kimaskini

Dini ya kimaksini, kifikra ilovia,
Hujikuta yumkini, na dola yafadhiliwa,
Wakafanziwa uhuni, mjini kuchopolewa,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Viongozi majinuni, rahisi kununuliwa,
Wakishapewa hamsini, mfukoni wanatiwa,
Hapo jua kwa yakini, waumini mwapotea,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Waumini hili guni, lazima kulikataa,
Hamna umaskini, huo unaodaiwa,
Mwaweza yenu kughani, na dini ikachanua,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Dola haina auni, dini imeshakataa,
Iweje leo amini, eti wanawasaidia,
Au huku ni kurubuni, motoni kuja ingia?
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Dini iliyo makini, sayansi itatumia,
Mtaji ikishaini, taratibu itakua,
Viongozi mkiwini, malengo wanaojua,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Ni tajiri sana dini, waumini kodi watoa,
Zaka wakizisaini, baitul mal yajaa,
Sadaka za waumini, bilioni zafikia,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Na kilicho mashakani, viongozi walokua,
Wengine ni mashetani, dini wameivamia,
Mayahudi na zayoni, wataka kututumia,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Wapatikane yumkini, viongozi wa kufaa,
Wakaikamata dini, kuleta yenye manufaa,
Indiketa hawaoni, waliokwishatutangulia,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Haijawa yumkini, dola kujatusaidia,
Yenyewe imashakani, mengi imeshalemewa,
Hata kadhi kutuhini, hazina inayo njaa,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

Waislamu sikieni, nyie fakiri hamjawa,
Haya ya watu maoni, sio ukweli nawambia,
Amkeni, amkeni, kutawala Tanzania,
Dini ya kimasikini, hufadhiliwa na dola!

No comments: