Sunday, November 6, 2011

Nipepee

Nipepee
Joto limezidi
Nipate kupoa
Jasho likipungua
Hamu ya kula,
huenda ikanijia.

Kweli njaa nasikia,
lakini joto limezidi
Hamu imepungua
Sio nafanya ukaidi
Ubaya sikuzoea
na ahadi ni ahadi.

Au pengine tusubiri
muda unavyokwenda
joto litapungua
hamu kunirudia
na ashiki kusikia
kula nikajaridhia.

Joto siku ungechagua,
Mihadi kutoingilia,
Mashtaka kuzuliwa,
wewe muuaji wa raha,
Na siku ukiamua
kuja kwetu kuingia
Mwombe naye mvua
mfuatane naye
Utangulie kuondoka
baridi akatanua.

No comments: