Monday, September 13, 2010

Kwanini usimwambie ?

Maneno ulonambia, nimeyaweka akiba,
Moyoni yajichimbia,kungoja yako haiba,
Nimeshalipenda ua,nakabidhi yote huba,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Na mshale wa mahaba,moyoni umeniingia,
nalia japo libaba, kila nikifikiria,
lini nami ntashiba,mikononi ukachanua,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Kooni umenikaba, dama nakufikiria,
Naomba nusura toba, wewe kunisaidia,
Hapanayo kwangu tiba,ila yangu kuridhia,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Kwangu ni kama nasaba, jinsi 'navyokuchukua,
Kwalo sinalo ghiliba, shaka moyoni ondoa,
Daima nitakubeba. wala sintokuachia,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Ninaomba yako huba, siha kuniongezea,
Nitakukuza habiba, ukubwani kuingia,
We dhahabu sio shaba, na utazidi kung'aa,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Sishibi yako haiba, hata kutwa kukuangalia,
Kifua chako kimeshiba, napenda kukichezea,
Kiuno chako cha mwiba, napenda kukishikilia,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Mdomo wako kiriba, napenda kuufungua,
Na ulimi kuuziba,joto kukupumulia,
Nitashiba, utashiba,hamu zitatuishia,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Nitakutoa ujuba, uke ukaufurahia,
Pumzi nitakukaba,raha ukaisikia,
Siri ni kwenye mkoba, mimi na wewe twajua,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

Penzi kama la kuiba, halali litajakuwa,
Zitapungua dharuba, wawili tukitulia,
Kwenye cha kwetu kijumba, mahala palipotulia,
Huntazami ukashiba, kwanini usimwambie ?

No comments: