Sunday, October 7, 2012

Watoto tusiachie



Jamani angalieni, watoto kuwaachia,
Waifanye kazi gani, kama si kututezea,
Wanayo akili nuni, dhikini wakatutoa,
Watoto tusiachie, kuyafanza ya wakubwa!

Huu kwetu mtihani, wapi sasa kuanzia,
Kwa sharubu wasomeni, na macho kuyafumbua,
Hekima akiauni,  yafaa kuangalia,
Watoto tusiachie, kuyafanza ya wakubwa!

Historia kubaini, kwa chini waliokuwa,
Wa juu usiamini, uongo watauzua,
Ya kweli msibaini, uoza mkachagua,
Watoto tusiachie, kuyafanza ya wakubwa!

Dini zenu muamini, ukweli wa kuaminia,
Uchamungu ufanzeni, balaa kuyoyomea,
Na dua kuamini, haki zaweza amua,
Watoto tusiachie, kuyafanza ya wakubwa!




3 comments:

Unknown said...

Really good at composing

Unknown said...

😘😄😁😃😃 nzuri




Unknown said...

Show😮😯😦😧