Sunday, October 7, 2012

Jaribu kujitambua



Usiwe wa kutumiwa, bila ya kujitambua,
Dini yako kwanza jua, na amri inazotoa,
Na kisha elimu kuwa, mwanga inakupatia,
Jaribu kujitambua, kabla haujatumiwa!

Na watu ukitumiwa, ni malaya unakuwa,
Shahawa ukamwagia, na hata  usowajua,
Kisha hukugeuzia, wapendavyo kukutumia,
Jaribu kujitambua, kabla haujatumiwa!

Unakuwa changudoa, kiumbe mkosa haya,
Tena mkubwa malaya, kila kitu unajua,
Bei yako yapungua, kwa mtuma na shabaha,
Jaribu kujitambua, kabla haujatumiwa!

Thamani hutoijua, kiumbe ukichakaa,
Ukabaki unalia, kwa bure ulioua,
Kwa kushoto na kulia, ikakucheka dunia,
Jaribu kujitambua, kabla haujatumiwa!

No comments: