Sunday, October 7, 2012

Kitunze hicho kidogo


Kdogo kiangalie, kitakuja kukufaa,
Usiache utunziwe, haiaminiki dunia,
Ni wakorofi watuwe, lako thamani huvia,
Kitunze hicho kidogo, kikikuwa kikufae!

Mwenyewe kisimamie, mwingine kutoachia,
Hadi kikubwa kikue, na kampuni ikawa,
Ndipo kazi usomee, watunze wa kuajiriwa,
Kitunze hicho kidogo, kikikuwa kikufae!

Wenda wote wasifae, hata ndani walokuwa,
Watataka watumbue, hali wataka chanua,
Ili usichanganyikiwe, ni bora kusimamia,
Kitunze hicho kidogo, kikikuwa kikufae!

Chako usikiachie, mikono isiyotulia,
Ni nadra ikilee, hadi kikubwa kikawa,
Wanaka wapakue, kibichi kilichokuwa,
Kitunze hicho kidogo, kikikuwa kikufae!

No comments: