Sunday, October 7, 2012

Kazi hii ngumu sana


Wazee wajikongoja, kazi mnawaachia,
Kazi yao kubwabwaja, wasiolikumbukia,
Watakuja kuyataja, msiyoyatarajia,
Kazi hii ngumu sana, wazee zawatatiza!

Wasojifunga mkaja,  vipi mnawatumia,
Wajivalisha makoja, nakshi yaliyotiwa,
Mvi kwa useja, busara wamepakua,
Kazi hii ngumu sana, wazee zawatatiza!

Inabakia kioja, wenye kanzu kujivua,
Na kisha wakenda haja, hadhara kulikokuwa,
Wakajiona wajanja, gizani kujisaidia,
Kazi hii ngumu sana, wazee zawatatiza!

Wa mbili havai moja, muda unawangojea,
Ujanja mwingine chaja, watu macho hufungua,
Na wa kuja si wakuja, ili hali kajitambua,
Kazi hii ngumu sana, wazee zawatatiza!


No comments: