Wednesday, February 29, 2012

Moja uanyoipewa

MWANA unanishtua, kwa unayoniambia,
Iweje ikatokea, moja wewe kupokea,
Kisha ukatoa mia, na mgeni kumwachia:
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Umeshindwa kuelewa, uchumi ulojisomea,
Akilini umekua, mweupe watakatia,
Huu ujinga najua, si vingine kunambia:
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Huwezi kutoa mia, wewe moja wapokea,
Tena ukashangilia, na fahari kufanyia,
Na kisha kumzawadia, moja anayesaidia:
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Utaahira nahofia, nyumbani umeingia,
Kila nikiangalia, si vingine nawambia,
Sasa nataka kujua, hayo misyonambia:
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Wa wapi mwawatumia, wataalamu walokuwa,
Nini wamesomea, na kama haya wanajua,
Au wanawapatia, kwa wenzao kuwanunua ?
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Angefufuka radhia, haya angeyakataa,
Majuha angewaambia, mwakubali nunuliwa?
Mwashidwa kufkiria, katika hii dunia:
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Katika hii dunia, kama mpya imekuwa,
Asia mgeingia, mengi mngeyavua,
Yapo ya kumalizia, na kisha kuendelezea,
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Mapya mngeyazua, ya wengi zaidi kufaa,
Na sio kuzainiwa, wachache yakawafaa,
Wanangu mnapotea, ukweli ninawaambia,
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Wanangu mnapotea, ukweli ninawaambia,
Utandawazi mwavia, na sasa mnaibiwa,
Pupa mmeingilia, wenyewe mpate jifaa?
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Nchi mwaiachia, kama malaya imekua,
Kila mtu mwachukua, hata wezi walokuwa,
Utakarifu wavaa, kumbe masheteani wawa,
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

Mwapasa kuangalia, tena sana kuchunua,
Wengine wanaowajia, Ibilisi wanakua,
Na nyie mkizuaa, nchi mwenda iua,
Moja unayoipewa, na wewe mia kutoa:
Aidha una kichaa
Au umelogwa pia
Au njaa wapagawa
Ya shetani ilokuwa
Na mwepesi kuja ua
Na kisha ukafukia
Bila ya watu kujua!

No comments: