Sunday, February 5, 2012

Msubiri maendeleo

Ni sera za waishiwa, kutwa kiguu na njia,
Huko mnakoingia, mlango wa nyuma watoa,
Kila mnachokipewa, mara kumi wachukua,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Laiti ningelikuwa, rais wa Tanzania,
Safari ningekataa, ila kwa inayolipiwa,
Nauli akaitoa, mwalikaji alokuwa,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Umaskini twajitia, kwenda wafuatilia,
Vyetu wanaochukua, mlango wa nyuma kupitia,
Kisha kutuhadaa, kwa pipi za chandalua,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Kisha kutuhadaa, kwa pipi za chandalua,
Na neti kututumia, za kutukinga malaria,
Hali wao waopoa, trilioni kuchimbua,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Nchi inayotegemea, wengine kuendelea,
Masharti huvaa, saizi isiyokuwa,
Na kondomu hugawiwa, kafanzeni mtapoa,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Mali asili zajaa, akili tunaziua,
Misaada sio dawa, ila ni kubwa balaa,
Tunazidi kulemaa, na siasa kufubaa,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Mwenzangu hebu chungua, upya twatawaliwa,
Lugha inayochakaa, bado tunaitumia,
Yetu tunaiachia, wengine kusaidia,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Hebu tazama Ulaya, wahandisi wamejaa,
Kijiweni wanakaa, ajira zimepotea,
Tunashindwa fikiria, jinsi ya kuwatumia,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Muda unaishilia, hadi wakajatengemaa,
Hapo ikishafikia, fursa imepotea,
Na kula anayezubaa, hujikuta Kwenye njaa,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Watu wanapigania, uongozi kuchukua,
Sasa nawaambia, wote hao kukataa,
Watoto tutachukua, viongozi kuja kuwa,
Msubiri maendeleo, nje yaje kutokea,
Hulala mlango wazi, na wezi kumwibia,
Amkeni Tanzania,
Waloshiba wananjaa,
Misaada ni hadaa,
Yawafanza kulemaa,
Vigumu kuendelea!

Februari 6, 2012,
Dar es Salaam.

No comments: