Monday, February 27, 2012

Mkiongozwa na waongo

Mkiongozwa raia, na waongo walokuwa,
Njia mnaifungua, mabaya zaidi kuwa,
Ibilisi asifiwa, kwa uongo kuuzua:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!


Kwalo atawajalia, pasiwe wa kuwang'amua,
Majoho kuwashonea, ya utukufu kuvaa,
Pasiwe wa kuwadhania, kuutunga wanajua:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Hapa wakishafikia, uovu wote hujua,
Waweza kukukatalia, haikuumbwa dunia,
Na kuwa wameshushiwa, na kiongozi mzawa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Vyombo wakikabidhiwa, vibaya huvitumia,
Akili wakafumua, nyengine kuwapatia,
Wasiwe wa kujijua, kufanya yenye udhia:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Kama mbwa watakuwa, mabwana kutumikia,
Kwa furaha kuwabwkea, na wengine kugugumia,
Ya kheri yakapotea, ikabakia balaa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Waongo huweza ua, waseme hiyo ni dawa,
Mgonjwa aliyopewa, ndiyo iliyomkataa,
Au kuishi kakataa, kwani juu atakiwa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Nchi wataibomoa, kujgenga wakadhania,
Nguzo wanazotumia, uongo zilizojaa,
Vigumu kuyachukua, yote yenye manufaa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Kinachokujakubakia, ubabe na kujikwaa,
Si wa kutegemea, waongo waliokuwa,
Ni ukoma wawavaa, vyema mbali nao kukaa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Si wanaojitambua, mchezo wanadhania,
Majukumu walopewa, rahisi kuyachukua,
Kumbe wanatuchimbia, makaburi hai twawa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Vikao hujifungia, uongo kuupakua,
Wakishakujipikia, uongo kutugawia,
Na sisi tusiojua, kweli tukaitikia:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Hata tusipoujua, au mambo kuyaelewa,
Mola awaangalia, wasanii walokuwa,
Nao awakadiria, adhabu kubwa ikawa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Uwongo autambua, kabla haujatolewa,
Na wizi kaandikia, hesabu iliyokuwa,
Na dhuluma aijua, kabla haujazaliwa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Kumbe wanatuchimbia, makaburi twapumua,
Sio kwamba wakosea, hili vyema walijua,
Ila mbinu imekua, kutokujauliziwa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Ni nchi iliyolaniwa, ya waongo ilokuwa,
Husema wasiyojua, na kutosema wakijua,
Husema wakufufua, kumbe waenda kuua:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Hata wakijititimua, dunia huwaumbua,
Mbegu hazitochipua, na mimea haitomea,
Na kilichochanua, matunda hakitotoa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

Kiapo hujiapia, bila aibu wakawa,
Na kisha kuyaingia, yaliyoishakataliwa,
Na katiba kupindua, kwa nia wanazojua:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!


Ninakuomba Jalia, taifa kuangalia,
Warongo kuwaondoa, wakweli tukabakia,
Radhiyo kutushukia,
nchi ikabarikiwa:
Mwongozwapo na waongo, uongo waliosomea,
Mwishowe huwafanyia, wakauzusha uongo,
Wenyewe mmejiua, au ni kifaurongo,
Kufufuka mwatarajiwa:
Budi kuwapa msongo,
Kwa kuanzia usogo,
Pamoja na zao hongo,
Mnyanyue wenu ungo,
Wenyewe mkajirushia!

No comments: