Sunday, February 19, 2012

Husahau

Anayetoka pabaya, ni mwepesi kusahau,
Ikamwingia kinaya, ukadhania bahau,
Akasishiya kujitia, kwa yasiyo na nahau,
Husahau atokako, kiumbe alolaniwa!

Mwepesi kutumbukiya, kwenye nyingi dafrau,
Hajui kujizuiya, nukuu wala rukuu,
Mjanja wa kujitiya, ucha usio juzuu,
Husahau atokako, kiumbe alolaniwa!

Hushika palipoachiwa, awe juu kama buu,
Na kumshikiliya, wengine hujisahau,
Chini akadondokewa, na kugeuzwa mafuu,
Husahau atokako, kiumbe alolaniwa!

No comments: