Monday, February 27, 2012

Wanasiasa fuska

MADHAMBI yakiingia, yakazidi kujizaa,
Kwenye safu za dunia, wakubwa walikokaa,
Muumba hatochagua, nani wa kumuumbua:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Hasira humalizia, pale inapoanzia,
Mwenye hurruma akawa, kama mbogo elfu mia,
Sauti akapasua, hadi nyota kukimbia:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Husasan akijua, wanaoharibu ndoa,
Kwa zinaa kuingia, na wengine kutumiwa,
Majonzi makubwa huwa,
viumbe wema wakalia:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Siasa zinachafua, majumba yaliyotulia,
Hakuna salama ndoa, hali tete imekua,
Na baadhi ya mikoa, wanafunzi watumiwa,
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Hadithi yasimulia, Tabora kulikokuwa,
Wakubwa kutfutiwa, mabingi wapate poa,
Mutumaina akawa, mkuu awasimamia:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Amri alipopewa, akajua ni unaa,
Masikini watakiwa, thamani hawajapewa,
Hilo akalikataa, na akawabadilishia,
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Mabinti kawatwaa, wa wakubwa walokuwa,
Vyumbani walipotomea, wakubwa wakashangaa,
Majina wanayopewa, ubaba uliokuwa:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Ya wenzao waliokuwa, pamoja wanapokaa,
Haya kuyashtukia, adabu ikawajia,
Mama walimtimua, ila pepo yamngojea:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

Nchi hivi ikishakuwa, jua kwamba yaalaniwa,
Mitihani kungojea, midogo na mikubwa pia,
Na huruma kutegemea, Mola hatotusikia:
Taifa hulaaniwa, kati yao kuwa nao:
Wanasiasa fuska
Hupata watu wabaya
Kahaba wakachagua
Na wezi waliokuwa
Uongozi wakatwaa
Mambo yote ovyo kuwa
Mikosi pia balaa!

No comments: