Saturday, February 4, 2012

Nakupenda, usiache nikakuchukia


Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa kilicho chetu wananchi wewe ukatuibia

Katiba na sheria ukaanza wazi kuchezea

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa mamlaka na madaraka ya watu kutwaa

Nawe ukajidai wananchi eti walikuachia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa katiba ya historia wewe kuipindua

Ukubwa ukachukua ambao haujapewa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa mafisadi kuwatetea na kisha kuwalea

Moyo radhi hautakuwa na sintoyafurahia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa rushwa kila kona ukawa unairidhia

Haki za wanyonge sokoni zote kununuliwa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Na wabunge tuliyowapa kofia wakaivua

Ya serikali wakawa waivaa na kisha kuitetea

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Ikawa watuchuua kila kipindi kutununua

Na bei wakawa waijua rahisi tulivyokuwa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Ikawa watuchuua kila kipindi kutununua

Na bei wakawa waijua rahisi tulivyokuwa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kama Mbeya kujakua watu bure wauawa

Pasiwe wa kusaidia wala hatua kuchukua

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Watu ukajaamua wenye mali waliokuwa

N wanyonge na fukara wao ni viatu wakawa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Siwezi miye kwa hakika nikaja kushangaa

Mbeya wakijaamua mkoa wa Zambia kuwa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Utadhani si Tanzania mkoa huu ulivyokuwa

Yote mwanzo uliojaliwa yamekwishasambaratika

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Watu ukajaamua wenye mali waliokuwa

N wanyonge na fukara wao ni viatu wakawa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kwa viongozi mbalimbali kuja kupagawa

Wakaamua ya nazaa, wakaacha ya manufaa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Wenyewe tukianza kuibiana kwa zetu hadaa

Na kutumia kuhalalisha kwa katiba na sheria

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Kulipa wasiozalisha, wazalishao kufa njaa

Kisha wananchi Tanzania watumwa wetu wakawa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Uongozi kuja oza na wauvaao ikawa wanafubaa

Wakatwaa na kuchukua, bila chochote kutwingizia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Ubunifu na uvumbuzi ukazidi baadaye kuvia

Tusiwe na cha kuzalisha tunachojivunia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Wanasiasa kujifanya kila kitu wanajua

Wataalamu kudharau na kutokuwatumia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Viongozi kula kwanza kila siku wakaamua

Hata makombo wakatwaa na wengine kugawia

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Viongozi wengi wakawa sasa wananunuliwa

Na Wazungu wa Amerika nao pia wa Ulaya

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Siasa nazo utendaji kila siku kuja kuingilia

Wanasiasa wakaingilia mengine wasiyoyajua

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

Usiache na mimi ije siku nikakuchukia

Nchi ikazidi kupotea na ustawi ukawa wadidimia

Nchi kugeuka ya njaa, jaa, mikosi, nuksi na balaa

Nitalia

Utalia

Tutalia

Kujutia

Ya hatia

Tanzania!

Februari 4, 2012

Dar es Salaam.

No comments: